Mbinu za Kulipwa Zaidi
Mbinu za kulipwa zaidi kwenye sekta yeyote ni kufanya kazi kitaaluma. Ni mchanganyikio wa tabia, ujuzi, na maadili chanya yanayomfanya mtu aaminike na kuleta matokeo bora.
Katika ulimwengu wa leo, kazi za nyumbani zimebadilika kutoka kuwa majukumu ya kawaida hadi taaluma inayohitaji maarifa, ujuzi, tabia na maadili maalum na uwajibikaji mkubwa. Waajiri wanatafuta wafanyakazi wa nyumbani ambao si tu wanaweza kufanya kazi kikawaida, bali pia wale wanaoweza kuchangia kujenga mazingira bora ya familia zao.
Hayo ndo mahitaji na matarajio ya waajiri wote. Kazi ya mfanyakazi yeyote akiwepo wa nyumbani ni kujikita kwenye kutatua changamoto za mwajiri wake kwa kiwango kinachotakiwa pamoja na kuonesha tabia nzuri na maadili chanya kwa familia ili mwajiri aweze kuridhika na huduma na kuwa tayari kulipia hiyo huduma unayotoa katika familia yake au ofisini.
Tatizo kubwa la wafanyakazi wengi hufanya kazi kama wanalazimishwa au kama vile wanasaidia bure, kwa wafanyakazi wa nyumbani wengi hawachukulii hii kazi kama taaluma, hawana maarifa, ujuzi, tabia na maadili wala shauku, ari na hamasa (PASSION) ya kutaka kujifunza na kutatua changamoto za waajiri kitaaluma.
Wafanyakazi wengi wana mitazamo hasi kuhusu kazi za ndani, wengi hawana tabia njema, maadili chanya, ujuzi au maarifa ya kazi, na wanafanya kazi kana kwamba wanatoa msaada wa bure au wananyanyaswa.