Maendeleo Ni MimiUtangulizi
Utangulizi
Ndugu msomaji,
Karibu katika shule ya maarifa ya mabadiliko ya kifikra yanayotokana na historia ya maisha yangu ambayo yanalenga kukusaidia kubadilisha maisha yako kuwa bora kiroho, kiuchumi na kijamii kama nilivyoweza kubadili maisha yangu kwa msaada wa Mungu.
Historia yangu na uzoefu wangu ni ushuhuda tosha kwamba kila mtu amepewa nguvu na uwezo wa kuboresha maisha yake endapo atajitambua sawasawa na kusudi la Mungu alietuumba na kutuweka hapa duniani.
Ninatumia ushuhuda wangu kama shule ya kuwajengea uwezo wale wanaoanza au wanaoendelea na safari ya maisha ya mafanikio hapa duniani na baada ya maisha haya kama tunavyoelekezwa na Katiba yetu ya Mbinguni ambayo ni Biblia.
i
Joyce KiriaUtangulizi
Kwanza kabisa katika shule hii ninayokupa nataka niweke wazi mfumo ambao nautumia maisha yangu kila siku, ni mfumo wa Ufalme wa Mungu, kwa sababu iko mifumo mbalimbali kwenye jamii yetu mfano mfumo wa demokrasia, ubepari, ujamaa, na mingine hiyo yote inatokana na wanadamu.
Mifumo ya wanadamu inajaribu kutatua changamoto za binadamu hapa duniani kama vile mipango ya maendeleo, uchumi, huduma za kijamii, mahusiano ya kijinsia lakini bado hiyo mifumo haijafanikiwa.
Mfumo Mkuu kuliko yote ni mfumo wa Ufalme wa Mungu ambao uliletwa na Yesu Kristo. Hivyo mimi binafsi natumia mfumo huo ambao unapatikana kwenye Katiba ya Mbinguni (Biblia) kama mfumo wenye majibu ya changamoto zetu za kila siku hapa duniani na baada ya maisha haya.
Biblia ni kitabu cha mwongozo wa maisha yetu ya kila siku na chenye majibu yote ya maisha yetu kutoka kwa Mungu alietuumba na ambae anatujua kuliko tunavyojijua sisi wenyewe.
ii